SIMBA YATEKA TUZO YA WACHEZAJI BORA LIGI KUU (VPL)


Club ya Simba imeongoza kwa kutoa idadi kubwa ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu (VPL) kwa msimu huu 2017/18.

Simba imetoa wachezaji saba (7) wanaowania tuzo hiyo, ikifuatiwa na Azam na Yanga ambazo kila moja imetoa wachezaji watano (5) katika kinyanganyiro hicho.

Singida United inawakilishwa na wachezaji watatu huku wapinzani wao katika mchezo wa fainali ya kombe la TFF Mtibwa Sugar ikitoa wachezaji wawili wakati vilabu vingune vikitoa mchezaji mmoja na vingine vikikosa uwakikishi.

Aishi Manula, Emanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Asante Kwasi (Simba SC.

Kelvin Yondani, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa (Yanga SC).

Yahya Zayd, Razack Abarola, Aggrey Morris, Himid Mao, Bruce Kangwa (Azam FC).

Shafiki Batambuze, Mudathir Yahya, Tafadzwa Kutinyu (Singida United).

Shabani Nditi, Hassan Dilunga (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Habibu Kiyombo (Mbao), Hamis Mcha (Ruvu Shooting),  Awesu Awesu (Mwadui), Adam Salamba (Lipuli) , Mohamed Rashid (Tanzania Prisons), Marcel Kaheza (Majimaji), Eliud Ambokile (Mbeya City) na Ditram Nchimbi (Njombe Mji).

Sherehe za utoaji wa tuzo ya mchezaji bora VPL 2017/18 zitafanyika Juni 23, 2018 ambapo tuzo zingine pia zitatolewa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post