Club ya Arsenal ya England leo imetangaza kuingia mkataba wa udhamini na nchi ya Rwanda hivyo wataanza kuvaa jezi zenye nembo ya ‘Visit Rwanda’ upande wa mikononi kuanzia msimu wa 2018/2019.
Rwanda imeingia mkataba wa miaka mitatu na Arsenal kwa ajili ya kuhamasisha watu kutoka mataifa mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii ndani ya nchi ya Rwanda.
Kama hufahamu pia Rais wa Rwanda Paul Kagame ni shabiki mkubwa wa club ya Arsenal hivyo haishangazi sana kuona Rwanda wamevutiwa kuingia ubia wa kibiashara na Arsenal.