SALAMBA ATIMKIA SIMBA BAADA YA AZAM NA YANGA KUTOFIKA DAU



Mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba, ana asilimia kubwa ya kuichezea Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ni baada ya kumalizana na mabingwa hao wapya wa ligi.

Simba imefanikisha usajili wa Salamba baada ya kuwazidi ujanja watani wao wa jadi, Yanga wal­iokuwa wanaiwania saini ya mshambuliaji huyo kwa ajili ya kumtumia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga walikuwa wa kwanza kupeleka barua ya Lipuli ya kumuomba mshambuliaji huyo ili wamtumie kwenye mi­chuano hiyo ya kimataifa na kujibiwa kanuni zinawazuia Salamba kutua Yanga kuto­kana na kuzichezea timu mbili katika msimu mmoja, Stand United na Lipuli.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti la Championi limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba, tayari taratibu zote za usajili wa Salamba zimekamilika na kilichobakia ni msham­buliaji huyo kusaini pekee.

Mtoa taarifa huyo alisema, mshambuliaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuichezea Simba leo Jumatatu jioni baada ya mechi yao ya ligi dhidi ya Kagera Sugar.

“Salamba rasmi ni mche­zaji wa Simba, kwani maz­ungumzo yamefikia sehemu nzuri ikiwemo kukubaliana dau lake la usajili analolihi­taji ili asaini Simba.

“Salamba anasajiliwa Simba baada ya kupokea mapendekezo ya kocha kati ya wachezaji anaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao, hivyo tayari tumefanyia kazi map­endekezo hayo na msimu ujao atakuwepo kwenye sehemu ya wachezaji wetu.

“Uongozi wetu wa Simba bado unaendelea na usajili kwa kufuata ripoti ya kocha wetu na kikubwa hatutaki kui­ingilia ripoti yake kwa kufanya usajili,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Salamba kuzungumzia hilo alisema: “Mimi siwezi kuzungumzia lolote katika hilo kama una­vyofahamu mimi bado mche­zaji halali wa Lipuli mwenye mkataba.

“Hivyo, hilo suala langu la mimi wapi ninasaini lipo kwa viongozi wangu ambao wanafanya mazungumzo na baadhi ya timu zinazonihi­taji.”

Alipotafutwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Selemani Ma­tola kuzungumzia suala hilo, alisema: “Zipo timu nyingi zilizoonyesha nia ya kum­hitaji Salamba, lakini kujua wapi anakwenda ni suala la kusubiria kama likikamilika tutaweka wazi kila kitu.”

Kwa upande wa uon­gozi wa Simba alitafutwa Kaimu Rais, Idd Kajuna kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa, lakini pia ali­tafutwa Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, Said Tully akasema: “Tunatarajia kuanza kuifanyia kazi ripoti ya kocha kesho Jumatatu (leo) ili kujua mapendekezo ya wachezaji na baada ya hapo tutaweka wazi kila kitu.”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post