MWAKA WA TABU YANGA


Yanga imemaliza ligi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL 2017/18 ikiwa na alama 52 nyuma ya Azam yenye pointi 58 na mabingwa Simba ambao wanapointi 68.

Azam imeichapa Yanga 3-1 katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara, mchezo huo ulikuwa unaamua timu ya kumaliza nafasi ya pili kati ya Yanga na Azam.

Ni msimu mgumu kwa Yanga ndani na nje ya uwanja, ndani ya uwanja Yanga ilianza kupoteza dira yake baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu George Lwandamina, ilijikuta ikishindwa kupata ushindi katika mechi tisa mfululizo kwenye mashindano yote.

Mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Simba na matumaini ya ubingwa kuanza kufifia, baada ya kufungwa na Simba ikapoteza mechi nyingine tatu mfululizo kwenye mashindano yote.

Nje ya uwanja Yanga inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi, wachezaji, benchi la ufundi na baadhi ya viongzi (waajiriwa) wanadai malimbikizo ya mishahara.

Hadi msimu unamalizika  Yanga imepoteza michezo sita (6) ya VPL jambo ambalo ni mara chache kuliona kwa vilabu vinavyowania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Mechi ambazo Yanga imepoteza msimu huu 2017/18

Mbao 2-0 YangaSimba 1-0 YangaTanzania Prisons 2-0 YangaMtibwa Sugar 1-0 YangaMwadui 1-0 YangaAzam 3-1 Yanga

Huu ni mwaka wa tabu ulioambatana na majanga kwa Yanga, kigi kuu imemalizika huku bingwa mtetezi akiabishwa kwa vichapo.

MPENDWA MSOMAJI WA BLOG YETU YA MPEMBA BLOG, KUTOKANA NA SHERIA MPYA YA SERIKALI YA KUSAJILI BLOG YETU KWA MUDA MFUPI HATUTOPATIKANA , HIVYO TUNAKUOMBA U DOWNLOAD APP YETU ILI UWEZE KUZIPATA HABARI ZETU KIURAHISI

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post