Mke wa P Funk Aapa Kupambana na Kajala Anayetaka Kuvunja Ndoa yao


MKE WA prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, Samira amefunguka kuwa licha ya kukutana na mitihani mingi ndani ya ndoa yake lakini kamwe hatokubali kuondoka nyumbani kwake na kumuachia nyumba muigizaji Kajala Masanja ambaye ni mzazi mwenziye na mume wake, kama alivyokuwa amepanga awali na atapambana naye. 

 Akizungumza kwa uchungu sana, Samira alisema kila uchwao anakutana na kashfa nyingi zinazomhusisha mumewe na Kajala lakini ameaua kukomaa na ndoa yake. 

“Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke,” alisema Samira.



Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana mara na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post