Kinachoendelea kuhusu uhamisho wa Griezman kwenda Barcelona, Atletico yatoa onyo




Image result for griezmann
Kuna kila dalili kwamba jezi namba 7 msimu ujao katika klabu ya Barcelona ikavaliwa na Antoine Griezmann, pamoja na jitihada za Atletico kutaka kumpa mkataba mpya lakini juhudi hizo zinaonekana kukwama, namba 7 ipo wazi Barcelona na tangu Arda Turan alipoondoka inaonekana kuachwa kwa ajili ya nyota ajaye.
Katika mkataba wa sasa wa Antoine Griezmann na Barcelona kuna kipengele cha mauzo ambacho kinaweza kumfanya Griezman kuuzwa katika timu nyingine kama timu hiyo itakuwa tayari kutoa kiasi cha £100m.
Raisi wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amethibitisha kwamba kulikuwa na mawasiliano kati yake na wawakilishi wa Antoine Griezman mawasiliano ambayo yalifanyika mwaka jana mwezi wa 10.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kuhusishwa na usajili wa Griezman kwani mwaka jana walijaribu kufanya jaribio kama hili hili japo lilikwama na klabu ya Atletico Madrid kutishia kuiburuza Barca katika mahakama ya FIFA.
Uhusiano wa Griezman na wachezaji wa Uruguay kama Martin Lasarte, Chory Castro, Diego Ifran na Diego Godin unamfanya pia kuwa karibu na nyota mwingine wa Uruguay anayekipiga Barcelona Luis Suarez.
Samuel Umtiti naye yuko karibu na raia mwenzake huyo wa Ufaransa na katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni alisema kwamba kama kutakuwa na nafasi kwa Griezma kwenda Barcelona baasi atafurahi.
Kwa sasa Griezman analipwa kiasi cha £15m kwa mwaka na Atletico Madrid wanataka kuongeza hadi ifikie £20m katika mkataba mpya, lakini Griezman inasemekana amekataa mkataba huo mpya Atletico.
Wakati Barca wakiendelea kupush uhamisho huu utokee, mkurugenzi wa Atletico Madrid bwana Miguel Angel Gil Marin ameibuka na kusema wamechoshwa na tabia wanayoifanya Barcelona kuanzia viongozi hadi wachezaji kwa namna wanavyomzungumzia Griezman na wamewaambia waachane na hilo suala kabla Atletico hawajachukua hatua kubwa zaidi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post