Baadhi ya wanachama wa Simba wanalalamikia katiba ambayo imepitishwa hivi karibuni na ipo kwenye taratibu za kupelekwa kwa msajili, katiba hiyo ambayo inaruhusu 49% za hisa apewe mwekezaji huku wanachama wakibaki na 51% imeanza kupingwa.
Wapo pia ambao hawakubaliabi na kanuni kwamba Rais wa klabu awe na elimu angalau kuanzia degree na kuendelea jambo ambalo lumetafrisiriwa ni kutaka madaraka yawe kwa ajiki ya watu wachache.
Manara amesema yupo tayari hata kutengua swaumu kwa ajili ya kupambana na watu wachache wenye lengo la kuivurunga Simba.
“Moja ya majukumu yangu ni kulinda image ya Simba, nikiona kuna mswahili anajaribu kuchafua image ya klabu ni wajibu wangu kumjibu. Natoa onyo kwa mara ya mwisho kwa kuwa mwezi huu ni wa Ramadhani tusije kuharibiana swaumu , yeyote mwingine akiendelea sitojali Ramadhani, mimi kujitengua swaumu kuja kulipa baadae sioni shida.”
“Nitapambana na ‘mdudu’ yoyote atakaejaribu kuiharibu Simba katika kipindi hiki, ninauwezo wa kusema kuliko mswahili yeyote aliyepata kuzaziliwa katika nchi hii. Ninauwezo wa kufyatuka kila aina ya neno.”
Watangazaji wa Leo tena wamemuomba Manara kuwa mvumilivu katika kipindi hili cha Ramadhani na kuwavumilia kila jambo ili asiharibu swaumu yake jambo ambalo ambalo baadaye Manara aliridhia, “sawa nimewaelewa.