Benki hutuma zaidi ya ujumbe mfupi
wa simu kila sekunde ikidhihirisha kwamba watu hutengemea simu zao aina
ya Smartphone kuliko tarakilishi kusimamia pesa zao.
Hapo awali
programu tumishi zilikuwa zikiwaruhusu watu kuangalia masalio yao na
huduma zote walizozifanya hivi karibuni kwenye benki, lakini kwa hivi
sasa programu hizo zinatumika mara kadhaa kutekeleza huduma ngumu zaidi
kama vile za mwenye akaunti kutaka benki kumkata pesa maalum na
kukabidhi mtu au kampuni fulani iwapo ana mkopo, utumiaji wa fedha kwa
marafiki na kazi nyingine za shughuli za usimamizi.Utafiti umebaini uongezeko la utegemeaji wa teknolojia kwa kufanya bajeti.
Hii ni baada ya benki kubwa ya Standard Chartered kuwafuta kazi wafanyikazi wake 285 wakidai kwamba ni mpango wa 'kuwahimiza' watu kutumia tecknolojia ili kuimarisha kazi zake katika kila huduma za benki hiyo.
Lengo la benki hiyo ni kuzihamisha asilimia 80 za huduma zake kwa matawi yasiokuwa na ofisi ifikapo mwaka 2020.
Imewekeza sana kwenye mitandao , huduma za simu na huduma za video benki kando na mashine za kuwekeza amana kwenye benki.
Benki za Kenya zinajaribu kupunguza matumizi ya fedha kwa kuimarisha huduma zao za kimtandao ili kuongeza udhibithi wa viwango vya riba uliopunguza pengo kutoka kwa biashara zinazoongoza kiuchumi.
Benki zimewekeza mabilioni ya pesa katika teknolojia ya taarifa na mawasiliano (ICT) inayotumika kuimarisha huduma za kutumia simu za mkononi na huduma za benki za mtandaoni. Mfumo huo umeimarisha kuongeza idadi ya wateja wake, bila wateja hao kuongezeka kwenye matawi mapya ya mabenki kama ilivyokuwa hapo awali.
Tanzania miongoni mwa nchi uchumi utakua kwa kasi zaidi duniani
Vijana wana mchango gani kwa uchumi wa Nigeria
Tecknolojia inabadili jinsi benki inavyotoa maelezo yake na uwasilishwaji wake.Benki nyingine tayari zinatoa maelezo kamili ya kumueleza mteja lini na kwa kiwango gani ambacho mtu hulipa kila mwezi na malipo yote yanayotolewa kwenye akaunti ya mteja na hata kiwango cha fedha kilichosalia kwenye akaunti zao wanafahamishwa.
Miaka 20 iliyopita , kiwango cha matumizi ya simu za mkononi barani Afrika zilikuwa kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na mabara mengine.
Huku mataifa mengine ya magharibi yalipokuwa yakiimarisha huduma za kimitandao ,Afrika bado haikuwa na ufahamu wowote kuhusu benki za mkononi, lakini hivi sasa bara la Afrika linaongoza kwa matumizi ya huduma za simu kwa kutuma pesa na huduma za benki.
Mataifa yanayoendelea kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2016 matumizi ya simu aina ya smartphone zilitumika kwa asilimia 28 ikilinganishwa na asilimia 77 Kaskazini mwa Marekani.Lakini imekadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2020 itaongezeka kwa asilimia 50.
Shirika la fedha la duniani, IMF limesema mwaka 2018 ndio mwaka utakaoshuhudia ukuaji mkubwa wa kiuchumi duniani tangu 2011.
Tags
Teknolojia