Siku kadhaa zilizopita msanii Gigy Money alimwaga povu baada ya kufanyiwa mahojiano na Ayo Tv na aliongea kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na mzazi mwenzake Mo J na moja kati ya vitu alivyozungumza ni kuwa mtoto sio wa Moj.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Gigy Money ameomba msamaha kwa mashabiki zake na watu wake wa karibu kutokana na kile alichokiongea kwenye mahujiano hayo .
”Sometimes mnajua hasira inaharibu vitu vingi. My last interview I was so angry, nimeongea mpaka kuptiliza so kwa wale nnaofanya nao kazi, nawaomba radhi. Kwa wale wanaonichukulia kama kioo cha jamii, wajue kwamba life is a journey and I’m learning with every step and to my fannnns, yani wapenzi wa dhati, asanteni for your love and support. Watch this space so mnajua Mama Myra sio wa mchezo mchezo. It will only get better.”