Wigi Lamuumbua JDee Lamvuka Ghafla Akiwa Stejini Mwenyewe Anena Haya


Mwanamuziki Lady Jaydee amezungumza ishu ya wigi kumvuka ghafla wakati akicheza.

Kitu hicho kinaonekana katika video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Anaweza ambao amemshirikisha msanii mkongwe kutoka nchini Jamaica, Luciano.

“Lilianguka, (anacheka) ilikuwa kwamba lilianguka chini, ni ajali kazini,” Lady Jaydee ameiambia Bongo5.

Hata hivyo ukitazama video ya wimbo huo kwa makini utagundua ulikuwa ni mpango wa makusudi ili Lady Jadee kuondoka katika scene hiyo na kupisha madansa katika video hiyo kuendelea na shughuli yao.

Katika hatua nyingine Lady Jaydee alizungumza kuhusu project mpya baada ya Anaweza.

“Kwa sababu ndio kwanza project imetoka hautakiwi kuongelea project ya mbele wanatakiwa wafurahie hii baada ya kuwa wamechoka basi tutazungumza kuhusiana na projet mpya,” alisema.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post