Kuna mvutano wa maneno unaendelea chinichini kati ya Barcelona na Real Madrid kuhusiana na utaratibu wa “Guard of Honour”. Hili ni gwaride maalum ambalo bingwa hupewa kwa wapinzani kukaa huku na huku na kuwapigia makofi.
Gerard Pique alitoa maoni yake kuhusu tishio la Madrid kugoma kufanya Guard Of Honour, Pique amesema “nitakosa usingizi”, akimaanisha kama Real Madrid hawatawapa heshima hiyo baasi hatalala kutokana na jambo hilo.
Upande wa Real Madrid ulikuwa kimya kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu Guard Of Honour, lakini sasa Sergio Ramos amefunguka kuhusiana na suala la Guard Of Honour na kuzungumza hatua ambacho kitawanyima raha Barcelona.
Ramos amethibitisha kwamba hawako tayari kufanya gwaride la heshima kwa Barcelona, Ramos amesema wao wanaungana na kocha wao Zinedine Zidane ambaye amethibitisha kwamba Real Madrid hawatafanya jambo hilo.
“Kwanza haimaanishi kwamba kutofanya jambo hili ni kukosa heshima, sisi tunafanya alichosema boss(kocha), hata kama watu wanajali sana kuhusu gwaride hilo na kocha akasema hapana baasi hatutafanya hivyo” alisema Ramos.
Inaonekana wanachofanya Real Madrid ni kulipiza kisasi kwani Barcelona walikataa kutoa heshima ya Guard Of Honour kwa Real Madrid katika El Classico mwishoni mwa mwaka 2017 baada ya Madrid kutwaa kombe la klabu bingwa dunia.
Japo suala la Barcelona kukataa likionekana kuwa na mashiko kwa sababu Barcelona wao wanaona sio haki kufanya Guard Of Honour kwa timu ambayo imeshinda mashindano ambayo wao hawakuwa sehemu ya washiriki.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA