Klabu anaiyoichezea Mtanzania Simon Msuva, El Jadida FC ya Morocco, imefuzu kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
El Jadid imefuzu kuingia hatua hiyo baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa leo dhidi ya AS Vita uliopigwa nchini Congo.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa mjini Morocco, Jadid walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Jadid inaingia hatua hiyo kwa kuwa na jumla ya mabao 3-2 katika Aggregate.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA