Ni vigumu sana Kusimama Katika HAKI Kwenye Dunia iliyojaa Uovu , Kwamaana Unapigwa Katika Kila Upande na Hata Waliotakiwa Kuzama Katika Maombi nao Wamekengeuka .
Ninapoitazama Kazi ya Msalaba Naelewa Kwanini Yesu Kristo alibaki Peke Yake .
Umepigana VITA ya Madini sikuona Waraka , Umejenga Ukuta Mkubwa Mererani Kulinda Rasilimali Yetu ya Tanzanite , Sikuona Waraka ,Umepigana Vita ya Rushwa,Umeanzisha Mahakama za Mafisadi sikuona Waraka Umepambana na Wazembe Maofisini sikuona Waraka, Umetoa Elimu BURE Sikuona Waraka , Umefufua Shirika la NDEGE, Unajenga Treni ya Mwendo Kasi (SGR) Sikuona Waraka. Umeanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Vyanzo Vipya Vya Umeme (Stigglers Gorge), Hatujaona Waraka.
Lakini Kama Haitoshi Umekomesha Mauaji ya Kutisha Ya Rai wasiokuwa Na Hatia kule Kibiti , Hatujaona Waraka ,Umekomesha Tabia Ya Askari kuvamiwa Na kuuwawa Vituoni wakiwa wanatimiza Majukumu yao Ya Kulinda Raia , Hatujaona Waraka.Nakumbuka Kulikuwa na Tabia Ya kutorosha Wanyama kwa Kuwapandisha Ndege, Leo Umekomesha , Hatujaona Waraka .
Lakini Niwakumbushe , Umeongeza Bajeti ya Ununuzi wa Madawa Na Vifaa Tiba Kutoka Bilioni 31 Mpaka kufika Bilioni 260 , sijawai Kuona Waraka .
Tangu Umeingia Madaraka Umeongeza Vivuko katika Maeneo Yote Yanayohitaji Vivuko vya Majini , pamoja Na Madaraja Ya Kupitia Juu kwa wananchi Kuvuka , Pamoja Na Ununuzi wa Meli Kubwa Za Mizigo Na kubeba Abiria, Sijaona Waraka.
Umeamisha Makao Makuu ya Nchi Kupeleka Dodoma ,Unaongeza Uzalishaji wa Umeme Huku Ukiwapelekea Wananchi Mpaka Vijijini , Umeongeza Nidhamu Serikalini Unaongeza AJIRA Kupitia Viwanda , Yote haya na Mengine Mengi Sijaona Waraka .
Leo Hii wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wanaunganishiwa Maji Mpaka kwa Mkopo , Sijaona Waraka.
Leo Hii Mtulia Kuhama Chama Ambapo Ni Haki yake Kikatiba Ndio Nimeona Waraka .Ninakusihi na Kukuomba nikiwa Mtumishi wa Mungu Ninae TAMKA mambo na Kutokea.
Ninaye Yaona Mambo Yasiyo ONEKANA kwa macho ya Mwili, Naiona Tanzania Mpya katika Uongozi wako.Shupavu.
Usifadhaike wala usihuzunike kwa Sababu Unayoyasikia LEO na Kuyaona Hutayasikia tena kwa jina la Yesu Krsito Mwana wa Mungu aliye Hai.
Nakwasababu Wamebadili Kusudi la Kufa kwa Yesu Kristo , na kupoteza maana ya Pasaka.Bwana wa Majeshi anakwenda Kupindua Meza zao Kama ilivyotokea YERUSALEM.. Endelea.
Ujumbe huu Ukawatie Moyo Watu Wote Wanaoipenda Nchi na Kukuombea kwa Roho na KWELI
Ni mimi Mtumishi Wenu
Paul Makonda
Niliyepewa kipande cha Dar es salaam
Tags
kitaifa