Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.
Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.
Profesa Anangisye amesema mwanafunzi anapokuwa amepandishwa kizimbani na akawa na kesi ya kujibu husimamishwa na akishamaliza kesi yake anarejea kuendelea na masomo.
Tags
kitaifa