Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako aondoe kigezo cha umri walichokiweka katika udahili wa wanafunzi kwa madai kitendo hicho kitapelekea kuwanyima elimu watoto wa kimasikini.
Hayo yameelezwa na viongozi wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT jana (Machi 26, 2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama chao yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT Jijini Dar es Salaam.
"Walichokifanya wizara ya elimu kwa kuweka kikomo cha umri wa udahili kwenye shule za serikali na binafsi kitapelekea kupungua wanafunzi wa elimu ya juu, kwa kuwa kikomo hicho kitawakwamisha hasa wananchi masikini wanaoishi vijijini na mijini katika kupata elimu. Kwenye hili tunamtaka Waziri wa Elimu aondoe kigezo cha ukomo wa umri kwasababu kigezo hicho kina kiuka Katiba", walisema viongozi hao. na kuongeza;
"Wametoa kikomo hicho bila ya kuwa na tafiti yeyote ambayo wamefanya wao kama Wizara au taasisi nyingine iliyopo nje ya serikali. Kuna athari kubwa katika kikwazo hicho kwa maana kuna watu walichelewa kupata elimu kutoka na maradhi, kusimamisha masomo kutokana na ada hivyo tunataka kigezo hicho kiondolewe ili watu wa aina wasikose kupata elimu".
Kwa upande mwingine, Viongozi hao wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT imeunga mkono waraka uliotolewa na Maaskofu wa Kanisa la KKKT nchini Tanzania na kuwataka viongozi wa dini nyingine wasikae kimya wafanye kama walivyofanya maaskofu.
“Ngome ya vijana inawapongeza sana kwa kutekeleza wajibu wao, ushauri wa maaskofu na maoni yao inabidi kuchukuliwa uzito wa hali ya juu, wamezungumzia kuhusu uhuru wa kutoa maoni, mauaji ya watu, katiba mpya, uchumi na ajira kwa vijana, ni mambo muhimu kwa watanzania wote bila kujali tofauti zetu kuyaunga mkono,.
“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema vuongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao.”
“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema vuongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao.”
Tags
Siasa