Pogba baada ya Zlatan kuvunja mkataba na Man United


Staa wa kimataifa wa Sweden aliyekuwa anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic jina lake leo limerudi kwenye headlines baada ya club ya Man United kutoa taarifa rasmi kuhusiana na kufikia maamuzi kwa makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba na Zlatan.

Zlatan imeripotiwa kuwa baada ya kuvunja mkataba na kuondoka Man United anakwenda kucheza Ligi Kuu Marekani MLS akiwa na club ya LA Galaxy, hivyo Paul Pogba ambaye amekuwa na mahusiano mazuri na Zlatan wakiwa wote Man United amemtakia kila la kheri.

Pogba ametumia ukurasa wake wa instagram kumtakia kila la kheri Zlatan kwa kupost video clip fupi wakiwa pamoja na kuandika “You’ll be missed Lion, wish you all the best 👊🏾🦁 @iamzlatanibrahimovic@manchesterunited #mufc “

Akimaanisha “Utakumbukwa Simba na kutakia kila la kheri”>>>Pogba

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post