Kompyuta Ndogo zaidi Duniani Yatengenezwa

Kompyuta Ndogo Zaidi Duniani Yatengenezwa


Kampuni ya IBM ya Marekani imetangaza kuwa imetengeneza kompyuta ndogo zaidi duniani ambayo ni ndogo zaidi kuliko kidonge kikubwa cha chumvi.

Taasisi hiyo IBM imefahamisha kuwa  kompyuta hiyo ina upana wa milimita 1, inaweza kuchunguza, kuchambua, kutuma na hata kutekeleza data.

Kompyuta hiyo inatumia betri ya nishati ya jua (Solar) ina kumbukumbu iliyotulia isiyo na mpangilio maalumu SRAM, na inafanya mawasiliano kupitia LED.

Kampuni hiyo imeonesha kompyuta hiyo kwenye mkutano wa Think 2018 ulioisha March 22 huko Las Vegas, Marekani, itawekwa kwenye bidhaa ili kurekodi ujumbe mbalimbali kuhusu uzalishaji wa bidhaa hizo. Teknolojia hii itakuwa njia mpya ya kuhakikisha usalama wa vyakula, kuthibitisha bidhaa halisi na feki, na kurekodi viwanda vinavyozalisha bidhaa za anasa.

Kabla ya hapo, kompyuta iliyotengenezwa na chuo kikuu cha Michigan iitwayo “Michigan Micro Mote” yenye upana wa milimita 2 ilikuwa kompyuta ndogo zaidi duniani.


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post