Wimbo wa msanii Diamond Platnumz ‘Sikomi’ wamfariji na kumtoa machozi muigizaji Nisha baada ya mpenzi huyo kuonekana kupitia kipindi kigumu katika mapenzi na kutamani kuwa Bachela.
Hivi karibuni kumekuwa na stori kuwa aliyekuwa mpenzi wa Nisha amekwapuliwa na mwanadada Snura Mushi ambaye ndiye anatoka naye kimapenzi.
Hata hivyo muimbaji huyo amekuwa akikanusha hilo kwa kueleza wapo pamoja kikazi tu na si vinginevyo.
Wimbo huo ambao maudhui yake unazungumzia mapenzi kwa mtu ambaye ametendwa, unasikika katika video ambayo ameiposti Nisha katika ukurasa wake wa Instagram ambapo anaonekana akiliakwa uchungu.
Tags
Udaku