BREAKING:’Nondo alikwenda kwa Mpenzi wake’-Polisi DSM


Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum DSM, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi, Abdul Nondo hakutekwa. Aidha amesema uchunguzi umebainisha kuwa alikwenda Mkoani Iringa kwa mpenzi wake waliyekuwa wakiwasiliana muda wote wa safari.

“Polisi baada ya kupata taarifa hii tulianza ufuatiliaji ili kubaini ukweli, tulipokea taarifa kutoka jeshi la polisi Iringa kuwa Mwanafunzi huyo alipatikana mkoani humo wilaya ya Mafinga akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti mahali popote” -Mambosasa

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post