Usiku wa Jumanne ya March 13 2018 ni siku ambayo haikuwa nzuri kwa baadhi ya mashabiki wa soka duniani hususani wanaoshabikia Man United, kwani ndio siku ambayo Club ya Sevilla ya Hispania ili hitimisha safari ya Man United ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018.
Man United wakiwa katika uwanja wao wa Old Traford katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 2-1, magoli ya Sevilla yote mawili yalifungwa na Ben Yedder dakika ya 74 na 78.
Ben Yedder ameifunga Man United akitokea benchi dakika ya 72 akichukua nafasi ya Luis Fernando Muriel kutokea Colombia na dakika 2 baada ya kuingia akafunga goli la uongozi kwa Sevilla, goli pekee la Man United liemfungwa na Romelu Lukaku dakika ya 84 ya mchezo.
Kama hufahamu vizuri Wissam Ben Yedder ni raia wa Ufaransa aliyezaliwa August 12 1990 katika mji wa Sarcelles nchini Ufaransa na kuanza kucheza soka mwaka 2000 katika club ya Garges-les-Gonesse aliyodumu nayo kwa miaka 7.
Ushindi huo sasa Sevilla unampeleka robo fainali kwa jumla ya magoli 2-1, kwani mchezo wa kwanza waliyocheza Hispania ulimalizika kwa sare tasa ya 0-0, Sevilla ameungana na Real Madrid, Liverpool, Roma, Juventus na Man City waliyofuzu tayari robo fainali ya UEFA msimu huu.