Kauli ya Msemaji Mkuu wa Serikali Baada ya Kuulizwa Msimamo wa Serikali Kuhusu Matamko na Waraka wa Viongozi wa Dini


Waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi.

Mambo hayo kwa mujibu wa waraka huo ni Utekwaji wa watu ,utesaji, kupotea kwa watu, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, alipoulizwa msimamo wa serikali kuhusu waraka na matamko mbalimbali ya viongozi wa dini  alijibu kuwa   kwa sasa serikali haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.


Hata hivyo, Jana Rais Magufuli aliwashauri maaskofu nchini waanze kuhubiri ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi badala ya kuishia kukosoa na kulalamika .

Alitoa kauli hiyo akiwa katika halfa fupi jijini Dar es salaam ya uzinduzi wa  magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post