China na Korea Kaskazini zathibitisha Kim Jong-un ndiye aliyezuru China


Kim Jong-un's wife Ri Sol-ju shakes hands with Xi JinpingHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMke wa Kim Jong-un, Ri Sol-ju akimsalimia Xi Jinping
Baada ya siku ya uvumi wa siku nyingi, imethibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.
Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na China na Korea Kaskazini, ndiyo ya kwanza inayofahamika ya Bw Kim nje ya taifa lake tangu alipochukua mamlaka mwaka 2011.
Bw Kim alifanya "mazungumzo ya kufana" na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing, shirika la habari la China, Xinhua liliripoti.
China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya wachambuzi wanasema uwezekano wa wawili hao kabla ya mkutano mkuu wa Bw Kim na viongozi wa Korea Kusini na Marekani ulitarajiwa.
Bw Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.
Ziara hiyo ya Beijing inatazamwa na wengi kama hatua muhimu katika maandalizi ya Korea Kaskazini kuhusu mazungumzo hayo.
Wakati wa ziara hiyo, Bw Kim alimhakikishia mwenzake wa China kwamba amejitolea kuacha kustawisha silaha za nyuklia, kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua.
Hata hivyo, alisema atafanya hivyo bila masharti.
Kim Jong-un and Xi Jinping with their wivesHaki miliki ya pichaCCTV
Image captionRuninga ya China ilionesha video ya viongozi hao wawili wakiwa na wake zao
"Suala la kumalizwa kwa silaha za nyuklia katika Rais ya Korea linaweza kutatuliwa, lakini iwapo tu Korea Kusini na Marekani watajibu juhudi zetu kwa nia njema, kuunda mazingira ya amani na uthabiti na pia kwa kuchukua hatua za kusonga mbele kwa pamoja kutoka kwa wadau wote kuhakikisha amani inapatikana," Bw Kim alinukuliwa akisema.
Uhusiano na Beijing
Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, lilieleza ziara hiyo kama yenye umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na China.
"Ina maana kwa Korea Kaskazini kufafanua msimamo wake na kushirikiana na China, mshirika wake muhimu zaidi," msomu katika Pacific Forum CSIS Andray Abrahamian ameambia BBC.
A police officer rides his motorcycle patrolling near Tiananmen Square in Beijing on March 27, 2018.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMaafisa wa polisi walidumisha ulinzi mkali karibu na uwanja wa Tiananmen Square
"Uhusiano huo umekuwa ukidhoofika katika miaka mitano iliyopita na China imekuwa imetengwa kidiplomasia katika miezi kadha iliyopita," amesema.
"Kutoka kwa mtazamo wa Beijing, hii ni ziara ambayo ilifaa kufanyika kitambo sana."
Man watches Japanese news report about possible visit by North Korean leaderHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVyombo vya habari vya Japan vilikuwa vya kwanza kuandika taarifa kuhusu ziara hiyo mapema wiki hii
Kwa sehemu kubwa, hii ni ziara yenye maana kubwa kwa urafiki wa Korea Kaskazini na China, na ni ishara ya heshima pia, Fyodor Tertitskiy wa shirika la habari la NK News linaloangazia sana taarifa kuhusu Korea Kaskazini alisema.
"Wana mikutano miwili mikubwa kati ya kiongozi wao na mataifa mengine - mmoja na Seoul na mwingine na Washington - na pengine wanataka kuusikia msimamo wa China pia.
Demonstrators dressed as North Korean leader Kim Jong-Un (R) and US President Donald Trump (L) embrace during a peace rally in Seoul on November 5, 2017Haki miliki ya pichaED JONES/GETTY
Image captionWaandamanaji Seoul 5 Novemba, 2017 wakiitisha amani kati ya Marekani na Korea Kaskazini
KCNA wamesema Bw Xi pia amekubali mwaliko wa kuzuru Korea Kaskazini.

Marekani yaridhishwa na shinikizo

Bw Kim aliwasili akiandamana na mkewe, Ri Sol Ju, Jumapili na wawili hao waliondoka Beijing Jumanne alasiri, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.
Ziara hiyo ni ya karibuni kwenye msururu wa shughuli nyingi za kidiplomasia tangu Korea Kaskazini na Kusini zilipoanza kuimarisha uhusiano wao wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi iliyoandaliwa Korea Kusini.
China iliwasiliana na utawala wa Trump na kuwafahamisha yaliyotokea katika mkutano huo Jumanne, serikali ya Trump ilithibitisha.
"Tunatazama hili kama ishara nyingine kwamba kampeni yetu ya kuweka shinikizo kali ndiyo inayozaa matunda na kufanikisha mazingira mwafaka ya mazungumzo na Korea Kaskazini," msemaji wa ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amesema.
Chinese policemen block a road as a procession believed to be North Korean officials pass near Diaoyutai State Guesthouse in BeijingHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPolisi wa China wakiwa wamefunga barabara kuruhusu msafara wa magari ya Korea Kaskazini kupita karibu na ikulu ndogo ya rais ya Diaoyutai, Beijing
Mwezi uliopita, Bw Trump alichukua hatua isiyo ya kawaida na kukubali mwaliko wa kukutana na Bw Kim baada ya miezi mingi ya uhasama na majibizano pamoja na Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora.
Mkutano huo wa Bw Kim na Bw Trump ukifanyika, basi Bw Trump atakuwa rais wa kwanza kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini akiwa bado uongozini.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post