Historia imeandikwa Mtwara na Yanga
Kwa mara ya kwanza katika historia, Yanga imefanikiwa kupata ushindi kwenye ardhi ya Mtwara ikicheza dhidi ya Ndanda FC baada ya kuifunga 2-1 kwenye mchezo wa VPL uliochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kabla ya mchezo wa leo (Februari 28, 2018) timu hizo zilikuwa zinecheza mechi tatu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Yanga haikuwahi kupata ushindi.
Ushindi huo wa Yanga dhidi ya Ndanda ni wa sita mfululizo kwenye ligi tangu iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi sita zilizopita.
Ruvu Shooting 0-1 Yanga
Azam 1-2 Yanga
Lipuli 0-2 Yanga
Yanga 4-0 Njombe Mji
Yanga 4-1 Majimaji
Ndanda 1-2 Yanga
Yanga imefikisha pointi 40 ikiwa nyumba
Tags
LIGI KUU VPL