AKILIMALI:Simba hata ikichukua Ubingwa, Lakini bado ni timu ya kawaida mno


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa anawapa Simba nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, endapo watapambana zaidi huku akisema bado ni timu ya kawaida mno.

Akilimali ameeleza kuwa, Simba imekuwa ikifanya vizuri msimu huu tofauti na miaka ya nyuma, lakini bado anaiona ya kawaida kwa kusema endapo watapoteza baadhi ya mechi zijazo, basi nafasi hiyo hawana.

Akilimali ametamba kuwa wao watapambana kwa kila liwezekanalo waweze kuzidi kuutetea ubingwa kwa tofauti ya pointi na si magoli, kutokana na watani wao kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga mpaka sasa.

Mpaka sasa Simba ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi, katika michezo 19 iliyocheza msimu huu.

Simba hivi sasa wako katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Stand United ya SHinyanga utakaochezwa Ijumaa ya wiki hii.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post