West Ham yamsimamisha kazi msajili wa wachezaji kwa kudai 'hatowasajili Waafrika zaidi'



Klabu ya Uingereza ya West Ham yamsimamisha mkurugenzi wake wa usajili wa wachezaji kwa kusema kuwa hatowasajili Waafrika zaidi

West Ham imemsimamisha kazi mkurugenzi wa usajili wa wachezaji Tony Henry kuhusu madai kwamba klabu hiyo haitawasajili teza wachezaji zaidi wa Afrika.

Gazeti la Daily Mail liliripoti kwamba Henry alisema kuwa wachezaji wa Afrika huzua fujo wasiposhirikishwa katika mechi

Katika taarifa, West Ham imesema kuwa haitavumilia ubaguzi wa aina yoyote ule na hivyobasi imemchukulia hatua mkurugenzi huyo kutokana na hatari ya madai yake.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limesema kuwa litachunguza rasmi swala hilo.

Taarifa iliendelea: Familia ya West Ham United inashirikisha kila mtu licha ya jinsia, umri, rangi , uwezo tabaka ama dini, kila mtu anakaribishwa

''klabu hiyo haitatoa tamko jingine lolote hadi pale uchunguzi utakapokamilika. Wafanyikazi wote hufunzwa kuhusu usawa na kutokuwa na upendeleo'', ilisema klabu hiyo.

Shirikisho la soka nchini Uingereza limesema kuwa lilishangazwa na matamshi hayo na kufurahia hatua iliochukuliwa na West Ham.

''Shirikisho la soka la Uingereza linashutumu maono kama hayo na hayataruhusiwa katika soka'', alisema.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post