Siku ya mwisho dirisha la uhamisho: Klabu za Uingereza zilitumia £150m



Baadhi ya wachezaji waliohamia katika timu mpyakatika dirisha la uhamisho la mwezi januari nchini Uingereza

Klabu za Uingereza ziligharamika katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari kwa kuweka rekodi ya matumizi ya £150m kufikia jumla ya £430m mwezi huu, kulingana na uchunguzi wa kampuni ya Deloitte.

Uhamisho uliogharimu fedha nyingi katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho ulijiri siku ya mwisho wakati mshambuliaji wa Dortmund Pierre Emerick Aubameyang alipojiunga na Arsenal kwa dau la uhamisho lililovunja rekodi ya klabu hiyo la £56m.

Kwengineko Tottenham, ilimsajili , Tottenham Lucas Moura kwa dau la £23m, huku Olivier Giroud na Andre Ayew wakielekea Chelsea na Swansea kwa dau la £18m huku siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho ikivunja rekodi iliowekwa 2011.

MATANGAZO

Matangazo ya uhamisho yaliendelea hadi mwendo wa saa tano usiku huku Eliaquim Mangala akiondoka ba kuelekea Everton kwa mkopo

Vilabu vikubwa tayari vilikuwa vimevunja rekodi katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari wakiipiku rekodi iliowekwa 2011 kwa £205m.

Wakati huo, Chelsea ilikamilisha uhamisho wa £50m ikimsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Fernando Torres, nayo Liverpool ikimsaini mshambuliaji wa Ajax Luiz Suarez kwa dau la £22.7m na kuilipa Newcastle £35m ili kumchukua Andy Carroll na hivyo kufanya matumizi ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kufikia £135m.

Miaka saba baadaye , washambuliaji wengine watatu waligonga vichwa vya habari huku uhamisho wa Aubameyang ukitegemea iwapo Dortmund itamchukua mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo huku Chelsea ikimnunua Giroud kutoka Arsenal ili kuchukua mahala pake.

Baadhi ya mikataba ilioafikiwa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho

Uhamisho uliokua ghali ulifanyika katika siku ya kwanza ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari wakati Liverpool ilipomsaini beki Virgil Van Dyk kutoka Southampton kwa dau la £75m.

Harakati za Leicester pia zilifanikiwa siku hiyo ya kwanza na kabla wiki ikamilike Everton ililipa kitita kilichovunja rekodi kumsajili mshambuliaji wa Besikitas Cenk Tosun kwa dau la £27m.

Baadaye Everton ilifanya usajili wa pili baada ya kumnunua Theo Walcot kutoka Arsenal kwa dau la £20m

Alexis Sanchez Aliondoka Arsenal na kuelekea Manchester United ikiwa ni mojawapo ya uhamisho ualiozungumziwa sana kabla ya kukamilika tarehe 22 Januari, huku Henrikh Mkhitaryan akielekea Arsenal.

Manchester City ilihusishwa sana na uhamisho wa Sanchez, lakini baadaye ikabadilisha mawazo na kuanza kumnyatia winga wa Leicester Riyad Mahrez, ambaye walimuachilia na kujiondoa katika siku ya mwisho ya uhamisho saa 24 baada ya kumnunua beki Aymeric Laporte kwa kitita cha £57m


Mikataba 10 ghali katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari

Kulingana na Deloitte, matumizi ya klabu za Uingereza kwa jumla katika msimu wa 2017-18 yanakadiriwa kuwa £1.9bn.

'Klabu kubwa sita Uingereza zafungua pochi

Huku kukiwa na ushindani mkali miongoni mwa klabu sita kuu katika ligi ya Uingereza, Chelsea ilimnunua Giroud na beki Emerson Palmieri kutoka Roma - kwa dau la £17.6m - huku Spurs ikimsajili winga wa PSG Moura.

Biashara ya mwisho iliofanywa na klabu hizo sita Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham - ilipanda kwa kitita cha £40,000 mwezi Januari 2017 hadi £265m mwaka huu.

Klabu hizo sita kwa kawaida zimekuwa zikiongoza katika matumizi ya kuwanunua wachezaji , lakini madirisha mawili ya mwisho ya mwezi Januari yanayonyesha kuwa ni timu hizo ambazo zimefanya biashara nyingi zikiweka ushawishi mkubwa katika haki ya matangazo ya runinga katika ligi hiyo kwa £5.136bn

Soko ililo ghali?


Grafu hii inaonyesha bei walizonunuliwa wachezaji wa ligi ya Uingereza mwezi januari ikilinganishwa na uhamisho wao wa awali.

Aubameyang awasili Arsenal

Arsenal ilikamilisha uhamisho ghali zaidi katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho wakati walipomsaini Aubameyang, hatua iliowafanya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter kutuma ujumbe 1,639 kwa dakika na zaidi ya ujumbe 280,000 kwa jumla kumuhusu.

Klabu hiyo ya London kaskazini ilitangaza usajili huo katika mtandao wa Twitter ikitumia #YoPierre, ambao ulisambazwa mara 77,000.


Ujumbe wa Twitter uliomtaja 'Aubameyang' ulisambazwa sana muda mfupi baada ya Arsenal kutangaza kwamba imefanikiwa kumsajili mchezaji huyo.

Je ni biashara nzuri kwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ambaye baada ya kumsaini mshambuliaji Alexandre Lacazette kwa kitita cha £46.5m mwisho wa msimu uliopita amevunja rekodi ya uhamisho wa klabu hiyo katika madirisha mawili yanayofuatana?

'Katika kipindi kama hiki, iwapo unaweza kupata mchezaji mwenye uwezo kama wake sio thamani mbaya', alisema mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Uingreza Ian Wright.

Atakapoanza kuzoea ligi ya Uingereza , ninatumai atafunga magoli ambayo Arsenal imekuwa ikiyataka wakati huu.

"Lazima afurahi na kinachoendelea . Hakufai kuwa na ukosefu wa washambuliaji''.

Mtaalam wa soka nchini Ujerumani Raphael Honigstein anaongezea: "Aubameyang ni mtu ambaye ataifungia magoli Arsenal, lakini sidhani kwamba akiwa pekee anaweza kuinua timu hiyo hadi kiwango chengine . Sio mchezaji wa aina hiyo.

Kwa kweli ni mchezaji mwenye kasi, ni mfungaji wa mabao na hatulii mahala pamoja.

Nadhani amepuuzwa na vilabu vikubwa kwa muda mrefu. Ramani ya ujumbe wa twitter uliomuhusisha Aubameyang wakati wa uhamisho wake London , ijapokuwa ramani hii hapa chini inaonyesha kuwa jina lake lilisambazwa sana nchini Nigeria na Thailand.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post