Harakati za kumpata bingwa wa kombe la shirikisho Tanzania bara (Azam Sports Federation Cup) 2017/18 bado zinaendelea na sasa mashindano hayo yamefikia hatua ya 16 bora.
Wakati mashindano hayoa yakinoga, vilabu sita vya ligi kuu tayari vimeshaaga mashindano baafa ya kupoteza mechi zaokatika hatua za mapema.
Mabingwa watetezi wa taji hilo walivuliwa ubingwa wao na Green Warriors kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya kufungana goli 1-1 katika dakika 90. Green Warriors inashiriki ligi daraja la pili.
Mbeya City, Kagera Sugar, Ruvu Shooting, Mwadui na Lipuli ni vilabu vingine vya ligi kuu ambayo vifuata nyayo za Simba kuaga mashino hayo yanayotoa mshiriki wa kombe la shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup).
Ligi kuu Tanzania bara imebakiwa na vilabu 10 ambavyo vilifanikiwa kuendelea na mashindano na vitacheza hatua ya 16 bora baada ya draw kuchezeshwa.
Vilabu vya VPL vilivyofuza 16 bora ya Azam Sports Federation Cup ni Yanga, Azam, Singida United, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons, Majimaji, Mbao, Ndanda, Stand United na Njombe Mji.
Vilabu vingine sita ni Dodoma FC, Polisi Tanzania, JKT Tanzania, KMC/Toto Africans, Kiluvya United (vyote daraja la kwanza) na Buseresere (ligi daraja la pili).