EPL yaweka rekodi mpya ya usajili, Jumatano pekee imemwagwa £150m

Usiku wa jana dirisha dogo la usajili la mwezi January limekamilika, vilabu vimefanya usajili mbali mbali na usajili mkubwa katika ligi ya EPL ukiwa wa Virgil Van Djik aliyejiunga Liverpool kwa £75m.

Kwa ujumla katika dirisha hili la usajili EPL vilabu vimetumia kiasi cha £450m hii ikiwa rekodi kubwa zaidi ya pesa ya usajili katika EPL kwenye dirisha la mwezi Janury.

Mara ya mwisho kwa vilabu vya ligi kuu soka nchini Uingereza kutumia pesa nyingi katika dirisha dogo ilikuwa mwaka 2011 kipindi Torres akijiunga Chelsea kwa ada ya £50m huku Andy Caroll akienda Liverpool kwa £35m.

Kwa mwaka huo pekee vilabu vya EPL vilitumia kiasi cha £225m kwa ajili ya kufanya usajili kiasi cha pesa ambacho safari hii inaonekana kimetumika mara mbili zaidi.

January hii ndio January ambayo kumefanyika usajili mwingi wa gharama kwani ukiacha Djik yupo Aubameyang aliyekwenda Arsenal kwa £57m, Manchester City nao wakimnunua Aymeric Laporte kwa bei kama ya Aubameyang.

Kwa siku ya Junatano tu pekee dirisha la usajili nchini Uingereza kulimwaga pesa zaidi ya £150m na kiasi hicho cha pesa kingeweza kufika hadi £200m kama Leicester City wangekubali kumruhusu Mahrez aende Manchester City.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post