Tatizo la Uvimbe katika sehemu za Uzazi za Mwanamke

JE, WAJUA UVIMBE KATIKA VIUNGO VYA NJE VYA UZAZI WA MWNAMKE?

Tatizo hili huwatokea zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa. Viungo vya nje vya uzazi vya mwanamke ambavyo huathirika  na tatizo hili la uvimbe ni mashavu au midomo ya uke na mlango au mdomo wa uzazi.

Mashavu au midomo ya uke kitaalamu huitwa ‘labia majora ambayo ni midomo ya nje ya uke, na labia minora ambayo ni midomo ya ndani ya uke. Mtomo wa kizazi kitaalamu huitwa Cervix.

Uvimbe katika viungo vya nje vya uke hutokea  hutokea tu au husababishwa na maambukizi. Uvimbe huu unaweza kuwa na maumivu au usiwe na mumivu. Uvimbe unaweza kuwa mdogo au mkubwa kutegemea na sehemu ulipo na muda tangu ulipoanza.  Mwanamke pia anaweza kupata tatizo la midomo ya ndani ya uke ambayo hurefuka na kujiona kama kero, hiyo ni hali ya ki maumbile na haina madhara.

AINA ZA UVIMBE

 

Uvimbe wa mashavu ya uke huwa unatokea kwenye tezi iitwayo “Bartholin gland”. Tezi hii huwa haionekani kwa macho na mojawapo ya kazi zake  ni kutoa majimaji  ya kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa.

Bartholine cyst: Huu ni uvimbe mgumu hutokea pembeni ya shavu la uke kwa ndani. Uvimbe huu mara nyingi huwa hauumi lakini huendelea kukua n kuleta shida wakati wa tendo la ndoa, na hutokea wenyewe. Uvimbe huonekana kwa macho au mwanamke anauhisi anaponawa ukeni au wakati wa kujamiiana.

 

Bartholine Abscess: Aina hii ya uvimbe ni jipu kwani nani yake huwa kuna usaha. Uvimbe huu huwa na maumivu makali huweza kupata homa, kushindwa kutembea vizuri na wakati mwingine uvimbe hupasuka. Maumivu husabbisha mgonjwa ashindwe kuendelea na mambo yake.

 

Dalili Zake

 

Dalili kwenye mdomo wa kizazi huwa kama ifuatavyo;

Kuhisi kitu kigumu kama gololi wakati mwanamke anapojisafishaKizazi kushuka chiniMaumivu wakati ama baada ya tendo la ndoaKutokwa na uchafu ukeni mara kwa mara unao ambatana na muwasho na harufu mbaya ukeniDamu kutoka baada ya tendo la ndoa au kuhisi kitu kinasukumwa kwa ndani wakati wa tendo la ndoa.

 

MATIBABU

James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya ya uvimbe. Tunapatikana Arusha, pia tuko nje ya Mkoa wa Arusha kwa Mawakala zetu. Unahitaji huduma, tafadhari tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post