NAMUACHA MKE WANGU KWAAJILI YENU!
“Nimeamua kumaucha mke wangu, nimekubaliana na nyinyi, kama nyinyi ndugu zangu hamumpendi basi sidhani kama na mimi naweza kuishi naye, nyie ni damu yangu sitaki kugombana na nyie sababu ya mwanamke!”
Patrick aliongea kwa kujiamini, ulikua ni usiku katikati ya chakula. Ni kitu ambacho hakuna mtu alikitegemea kwani siku zote alikua upande wa ndugu zake, walimkataa mke wake muda mrefu, kipindi cha uchumba lakini alilazimishia kumuoa.
Walishamfanyia vituko vingi ili amuache lakini wapi, alisimama na mkewe na hakuna aliyetegemea hasa katika kipindi hiki ambacho ndiyo alikua na wiki tu kajifungua mtoto wao wa kwanza.
Dada yake ambaye ndiyo alikua kimbelembele zaidi alinyanyuka na kushangilia, alitoka pale na kwenda chumbani kwa Kaka yake, kumgongea wifi yake ambaye alikua ananyonyesha mtoto na kuanza kumtukana kumuambia aondoke mule ndani kwani hatakiwi tena.
Mama yake alipiga vigelegele, wadogo zake wakiume walikua wakishangaa tu kwani wao walikua hawaingilii mambo ya Kaka yako. Baba yake alimuuliza kwanini anafanya hivyo, alisema ameamua kwani mkewe hapatani na Mama yake na hataki kukosa radhi za Mama.
Alimshauri kuangalia uamuzi wake huku akimuambia angalau angengoja mtoto akuekue lakini Mama yake alidakia, alianza kumtukana Baba yake na kumuambia anyamaze kwani tayari washamtafutia mwanamke mwingine na angemsaidia kulea mtoto, kwa mkewe ilikua ni kilio mara mbili.
Kwanza ndiyo alikuaamejifungua na kutokana na mimba yake kumpa tabu sana alilazimika kuacha kazi hivyo alikua akifukuzwa na mtoto wake huku akiwa hana kazi ya kufanya. Nyumbani kwao yeye ndiyo alikua anategemewa, usiku alikusanya vitu vyake taratibu huku akilia tu.
Asubiuhi Patrick alimpakia kwenye gari na kwenda kumkabidhi kwa wazazi wake Morogoro. Alirudi nyumbani na kukuta Mama akiwa na furaha, tayari walishamleta binti ambaye walitaka amuoe, Patrick aliwoamba wasubri kidogo ili wapange harusi ya kueleweka ambayo ndugu zake watahudhuria kwa furaha.
Aliwaambia inabidi kwanza afuatilie suala la talaka ili mkewe asije kuweka pingamizi kwani ndoa yao ilikua ya mke mmoja. Walimualewa na kumtaka aharakishe. Baba yake bado alikua akimsihi kuangalia uamuzi wake na kufikiri mara mbili lakini hakujali, alishaamua kuachana na mkewe ingawa alikua anampenda sana.
*****
Miezi mitatu baada ya Patrick kuachana na mke wake, kulikuja wageni, ni mchumba wa Dada yake Josephine ambaye alikuja kujitambulisha. Ni jambo ambalo lilipangwa muda mrefu. Josephine na mchumba wake walishakaa kwenye mahusiano kwa miaka sita na sasa walikua wako tayari kuoana.
Kama Kaka mkubwa alihusika kwa kila kitu, wageni walikuja na kupokelewa vizuri, walipangiwa siku ya kuleta mahari. Siku ya kuleta mahari ilipofika Patrick alibadilika, aliwaambia wagani kua hawawezi kupokea mahari. Kila mtu alsihangaa kwani kila kitu kilsiahapangwa, Baba yake alimtuliza lakini alisema hapana
Aliwaambia huyu kijana hawezi kumuoa Dada yangu, walimsihi kutulia lakini alisema hataki, kulizuka kavurugu mpaka wageni wakaombwa kuondoka nakupangiwa siku nyingine. Baada ya wageni kuondoka watu woe walimfuata Patrick na kumuuliza kwanini alifanya kile kitu cha kuwatia aibu.
Aliwajibu kuwa hataki Dada yake aolewe na yule mwanaume, anaona sio mtu mzuri na hafai katika familia yao, aliulizwa kwanini alisema macho yake tu yanaonyesha si mtu mzuri, alisema pia ana nywele ndefu anaonekana mhuni mhuni hivyo atamuumiza Dada yake.
Kwa Dada yake ilikua ni kilio tu, akisema hawezi kuachana na mchumba wake kwani wametoka mbali, anampenda sana na hayuko tayari kumuacha kwani alishavumilia sana na hakuna namna angeweza kupata mwanaume mwingine kwa umri wake wa miaka 31.
Patrick alimuambia usiwe na wasiwasi, siku iliyofuata alikuja na kijana mwingine ambaye alisema ni rafiki yake na kusema huyo ndiyo alitaka amuoe Dada yake. Kila mtu alishangaa na Dada yake aligoma kabisa kuolewa na huyo kijana.
Mama yake alimtishia kumuachia laana kwa kumharibia Dada yake ndoa, lakini bado alikataa na kusema kama anaolewa basi yeye asimtambue kama ndugu yake na siku ya harusi yake hatoenda. Dada yake alimuambia potelea mbali ni bora asiende lakini hawezi kuachana na yule mwanaume, Patrick alimuambia hata akiolewa hawatadumu kwani atahakikisha hawana furaha.
Siku na hatimaye wiki na mwezi ulipita kukiwa haijulikani wafanyeje, Patrick aliahidi kuharibu kila kitu akisisitiza Dada yake kuolewa na mwanaume anayemtaka yeye. Ilibidi kuitishwa kikao cha wazee ili waongee, alipoulizwa alisema yeye hana sababu ya msingi lakini hamtaki tu!
Mama yake alimuambia huwezi kumpangia Dada yako mtu wa kumuoa. Patrick alinyanyuka na kuwaambia wewe Mama na Dada ndiyo mlinifanya nikamaucha mke wangu, kwakua hamkua mkimpenda na hamkua na sababu zozote za msingi, sasa iweje mimi mnipangie lakini nyinyi hamtaki niwapangie?
Chumba kizima kilikaa kimya, Mama yake aliangalia chini kwa aibu. Patrick aliendelea. Kama kweli mlikua mkiniamulia kwakua mnanipenda sasa na mimi namuamulia kwakua nampedna sitaki aolewe. Dada yale alimfuata na kumuomba msamaha kwa kuingilia ndoa yake na kusema kuwa hawezi kufanya hivyo tena.
Mama yake pia alimsihi kuwasamehe kwani walifanya makosa kumuingilia katika ndoa yake. Patrick hakuwajibu, aliondoka akaingia kwenye gari, siku iliyofuata alirudi akiwa na mkewe pamoja na mtoto wake. Aliwaambia mimi si mpumbavu, sikumaucha mke wangu kwakua nampenda sana.
Nilijua kwa roho mbaya zenu mngeweza kumuua hata mtoto kwakua mnamchukia mke wangu, alipojifungua nikaamua nimpeleke kwao akahudumiwe kwa upendo, sasa ameshamaliza nimemrudisha. Kama mlivyosema hakuna kupangiana katika maisha sitaki mtu anipangie chochote.
Huyu ni mke wangu, ni familia yangu, sitaingilia maisha ya mtu lakini pia sitataka mtu aingilie maisha yangu. Ukigombana na mke wangu, ukimuudhi mke wangu ukimkasirisha mke wangu hata ukipita tu mbele yake akachukia, hata ukivaa nguo asipoipenda jua kuwa kwangu hutakanyaga tena.
Alisema hana kipingamizi tena cha Dada yake kuolewa. Dada yake alirudi kwa mchumba wake kumuomba waje tena lakini alikataa na kusema anafikiria kwanza, alimuambia sababu ya Kaka yake kukataa siku ile ili asiolewe.
Mchumba wake alikasirika zaidi kusikia tabia za mtu ambaye alitaka kumuoa, alimuambia hawezi kuoa mwanamke kama yeye ambaye anaweza kumchukia mwanamke mwenzake bila sababu ya msingi.
Alimuambia familia yake inaonekana ina kisirani hivyo itamletea matatizo. Aliachwa na sasa yupo tu ana danga huku na kule akiwa hana uelekeo! Patrick na mkewe wanaishi maisha yao raha mustarehe na Mungu kawajaalia mtoto wa pili!