Hali ya hewa yaleta hofu uwepo wa mechi kati ya Arsenal na Man City


Beast from the east ni msimu wa majira ya baridi kali nchini Uingereza ambapo katika msimu huu huwa kunakuwa na barafu katika sehemu kubwa ya Uingereza, mji mkuu wa nchi hiyo ndio huathirika zaidi na barafu hiyo.

Hali sio nzuri nchini Uingereza kutokana na barafu hiyo ambapo shule nyingi zimefungwa na barabara hazipitiki hali inayotilia mashaka uwezekano wa pambano kati ya Arsenal na Manchester City kufanyika.

Arsenal walikuwa waikaribishe Manchester City katika uwanja wao wa Emirates siku ya Alhamisi lakini sasa pambano hilo kuna uwezekano mkubwa lisifanyike japokuwa bado chama cha soka Uingereza (FA) hawajatoa taarifa kamili.

Kutoka Manchester ambao ndio mji ambapo Man City wanatokea hadi London usafiri mkubwa huwa ni treni lakini kwa hali ya hewa mjini humo inatia mashaka hata uwezekano wa treni kuweza kwenda London.

Kamati ya FA inatarajia kutoa taarifa kamili kama mchezo huo utakuwepo ama laa siku ya Alhamisi asubuhi lakini hali ya nje ya uwanja wa Emirates pia hairidhishi kwa sasa na hamna mazingira rafiki ya kucheza soka.

Mchezo kati ya Arsenal na Manchester City unakuja siku chache baada ya timu hizo mbili kukutana katika fainali ya michuano ya Carbao Cup ambapo Manchester City walibeba ubingwa wa michuano hiyo kwa kushinda mabao 3 kwa nunge.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post