Mtoto wa Kwanza wa Aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro Ajiua

Mtoto wa Kwanza wa Aliyekuwa Rais wa Cuba Amejiua
Taarifa iliyoshika headlines kwenye vyomba vya habari nchini Cuba ni kuhusu Mtoto wa Mwanamapinduzi na aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro, Fidel Ángel Castro Díaz-Balart, mwenye umri wa miaka 68 amejiua akiwa mji mkuu wa Havana.

Amekutwa amefariki February 1, 2018 na inadaiwa alikuwa anatatizwa na msongo wa mawazo. Castro Díaz-Balart alifahamika sana kama “Fidelito” na alikuwa mtoto wa kwanza wa rais huyo wa zamani wa Cuba aliyefariki dunia November 2016.

Alikuwa mshauri wa kisayansi wa Baraza la Serikali ya Cuba na alihudumu kama makamu rais wa Chuo cha Sayansi cha Cuba pia alifanya kazi kama Mwanafizikia ya nyuklia.

Gazeti rasmi la Serikali ya Cuba la Granma limeandika hivi

 “Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa ametibiwa na kundi la madaktari kwa miezi kadha kutokana na msongo wa mawazo, alijitoa uhai asubuhi hii,”

Runinga ya taifa imesema amekuwa akipokea matibabu miezi ya karibuni kama mgonjwa wa kutibiwa na kurudi nyumbani, baada yake kulazwa hospitalini kwa muda. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post