Baada ya mabao, sasa Messi aweka rekodi ya kugongesha mwamba

Baada ya mabao, sasa Messi aweka rekodi ya kugongesha mwamba

Dakika ya 37 Lionel Messi aligongesha mwamba wa juu la goli la Eibar, pamoja na kupiga mwamba huo lakini Barcelona wakaibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 unaozidi kuwakita kileleni.

Tukio la Lionel kugongesha mwamba limekuja na rekodi mpya ambapo sasa Muargentina huyo anakuwa amegongesha mwamba mara 14 na kwa sasa hakuna mwanasoka La Liga anayemfikia kwa hilo.

Rekodi ya kugongesha mwamba katika La Liga ilitambulishwa mwaka 2003/2004 na tangu kipindi hicho hakuna mchezaji ambaye aliyegongesha mwamba mara nyingi kama Lionel Messi.

Lakini mchezo wa Barcelona vs Eibar imekuwa kwa mara ga kwanza Messi anashindwa kuwafunga Eibar katika michezo saba waliyokutana japo bado anaongoza kwa ufungaji wa magoli akiwa na mabao 20 katika mechi 24 za La Liga msimu huu.

Kesho Lionel Messi atawaongoza wenzake katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya watakapokuwa ugenini nchini Uingereza kuikaribisha Chelsea.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post