Mgombea Ubunge Kinondoni aiomba radhi CCM kwa kuigaragaza vibaya alipokuwa CUF


Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amewaomba radhi wanachama wa chama hicho tawala kwa ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiwa CUF.

Mtulia ametoa kauli hiyo leo Januari 21, mwaka 2018 wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho wilaya ya Kinondoni.

Mwaka 2015, Mtulia alishinda ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, lakini Desemba 2 mwaka jana alijivua uanachama wa chama hicho na kuhamia CCM, hivyo kupoteza sifa ya ubunge. 

Hata hivyo CCM kilimpitisha kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Na Jackline Masinde na Pamela Chilongola,Mwanachi

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post