Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. ambavyo hujitokeza katika vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi.
Vile vile Chunusi hujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe ndipo hutoka kwa wingi kwa kijana huyu.
Nama ya kujitibu:
Kitunguu Swaumu:- Kitunguu swaumu ni moja ya dawa inayoaminika kuwa inaweza kutibu taizo hilo. Kwani kina nguvu za kuua bakteria mbalimbali na kuzuia magonjwa ikiwemo kutibu chunusi.
Ndimu/ Limao:- Limao na ndimu zinaVitamiv C kwa wingi amabyo ina uwezo wa kuua backteria kwa haraka wanaosababisha chunusi.
Asali Mbichi:- Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya asili ambayo husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi na maumivu ya chunusi.
Aspirin: – Aspirin inaweza kuwa ni moja ya dawa nzuri za chunusi. Chukua vidonge viwili au vitatu vya aspirin na utwange upate unga wake kisha ongeza maji kidogo upate uji mzito. Ila fanya tiba hii kwa mara moja kwa wiki.
Chumvi na mafuta ya zeituni:- Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafuta ya zeituni yandhibiti bakteria na huondoa sumu vitu ambavyo vinafanya kuwa dawa nzuri kutibu chunusi na matokeo ya chunusi.