"Safari hii mtatufunga wote" - Mbowe

Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Mbowe amefunguka na kusema kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa marudio katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha jeshi la polisi liandae magereza ya kutosha kwani watawafunga wote na kudai hawawezi kukubali kura kuibiwa.

Mbowe amesema hayo leo Januari 29, 2018 akiwa kwenye kampeni za CHADEMA Magomeni ambapo amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila polisi ni wepesi na hawawezi chochote sababu chama hicho kimeshapoteza mvuto kwa wananchi. 

"Yaani nyinyi polisi muachie CCM dakika tano tu wacheze ngoma siku ya tarehe 17 hawa jamaa ni weupe, na polisi ndugu zangu safari hii mtuandalie magereza mtatufunga wote haki ya Mungu safari hii haibiwi mtu kura hiyo nawaambia mtatuua. Kama tumeweza kupona risasi 38 sasa tupo tayari kwa lolote, haiwezekani wanaume na wanawake wa mageuzi tukafanywa sisi kama ni wake za mtu haiwezekani. Wabunge wetu wanafungwa, wanafukuzwa Bungeni, madiwani wanalazimishwa kuhama chama, kila siku viongozi wa upinzani ni polisi na mahakamani" 

Mbali na hilo Mbowe amesema endapo saizi watafanyiwa mambo ambayo walifanyiwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 basi mambo hayawezi kuwa mazuri.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post