Ozil ashauriwa na Baba yake kuachana na Ujerumani


Baba wa kiungo mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil amemshinikiza mchezaji huyo kuacha kuchezea timu ya taifa baada ya alichodai kuwa ni mashambulizi ya maneno kutoka kwa mashabiki wa nchi yake .

Mchezaji huyo na mwenzake Ilkay Gundogan waliingia katika sintofahamu na mashabiki wa Ujerumani baada ya kupiga picha pamoja na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan siku chache kabla ya kuanza kwa kombe la Dunia.

Ozil ana asili ya Uturuki na tukio hilo la kupiga picha lilitafsiriwa kuwa ni la usaliti kwa nchi hiyo na wengi wakimtuhumu kutofanya vizuri katika michezo yote ya kombe la Dunia .

“ Mimi ningekuwa ni yeye, ningesema sasa inatosha na kuachana na timu hiyo “. Amesema Mustafa, Baba wa Mesut Ozil.

“ Amekatishwa tama, ndiyo amekatishwa tama na mashabiki wake kabla ya kombe la Dunia wakiwa Austria, na hakujua ni sababu gani . Amecheza timu ya taifa kwa miaka 9 na muda wote imekuwa ikisemwa kwamba timu ikipoteza basi wachezaji wote wamepoteza, lakini sasa timu ikipoteza basi Ozil peke yake ndiye aliyewapoteza “.  Ameongeza Mustafa.

Ujerumani iliondolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia baada ya kushinda mchezo mmoja pekee dhidi ya Sweden huku ikufungwa 1-0 na Mexico katika mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa mwisho wa hatua hiyo 2-0 dhidi ya Korea Kusini. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post