WAZAZI WAMUUA MWALIMU KISA MATOKEO MABAYA

WASHUKIWA wawili wamekamatwa baada ya kukashifiwa kwa kumuua mwalimu wa shule ya msingi kaunti ya Kitui. Wawili hao wanazuiliwa huku uchunguzi ukifanywa dhidi yao.

Wambua Mwangangi na Chris Kyalo Muli wanasemekana kumuua mwalimu huyo baada ya shule yake kutoa matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka wa 2019.

Daisy Mbathe aliripotiwa kushambuliwa kwa panga kabla ya mwili wake kuteketezwa na washukiwa hao. Mbathe ambaye aliuawa Januari 6, 2020 alikuwa mwalimu katika shule ya msingi ya Ndooni.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post