Muhubiri mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili katika mkusanyiko wa kanisa lake akidai kwamba wadudu hao walibadilika na kuwa jibini kwa mmoja wao na kiungo kwa mwengine.
Kisa hicho kinajiri takriban miezi mitano baada ya Mnguni katika ibada ilioandaliwa na Muhubiri wa Nigeria TB Joshua, na kukiri kulingana na bwana Joshua kwamba kuwalisha watu haijaandikwa katika biblia.
Kanisa la bwana Mnguni lilichapisha katika mtandao wa facebook kuhusu kisa hicho cha kula mende mapema mwezi huu akisema kuwa muhubiri huyo alimwita mende kuja katika kanisa hilo.
Baadaye aliwaita wafuasi wa kanisa hilo kujitokeza mbele na kula....ndiposa ndugu wawili walijitokeza na kula pamoja...na walipokuwa wakila bwana Charles alihisi anakula jibini huku Bwana Eric akihisi kula kiungo, chapisho hilo lilisema.
Huku akizungumza maneno haya ''uwezo wa mungu uliwagusa wote wawili, kwa kuwa walipo'' , aliongezea.
Kanisa hilo pia liliripoti katika chapisho jingine kwamba muhubiri huyo aliliombea uwa la sumu , na baadaye mfuasi mmoja alilila ua hilo pekee na kulimaliza.
Nabii huyo aliyejitangaza alizua utata nchini Afrika Kusini 2015 baada ya kushutumiwa kwa kuwalisha nyoka wafuasi wake.
Mashtaka dhidi ya Mnguni yaliowasilishwa na shirika la kuzuia ukatili dhidi ya wanyama ,yalitupiliwa mbali mnamo mwezi Julai 2015 kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Tags
kitaifa