Madereva Daladala wa Kituo cha Mawasiliano Simu 2000 Wagoma


Madereva Daladala wa Kituo cha Mawasiliano Simu 2000 Wagoma Baadhi ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000 Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.

Mbali na hilo, wamesema ubovu wa barabara hiyo ya Mawasiliano ni sababu nyingi kwa madai ya kwamba magari yao yanaharibika kila kukicha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili walisema walianza mchakato huo tangu saa 11 alfajiri na kwamba wataendeleza hatua hiyo hadi mamlaka husika itakapotoa mwafaka w sinofahamu.

Mmoja wa madereva hao Abdulsalum Hamad amesema waliingia katika kituo kama kawaida lakini wakati wanataka kutoka wakaamriwa kulipa Sh 1000 jambo ambalo hawalukubaliana nalo.

"Baada ya kuamua kugoma kutolipa kiasi hiki walitushirikilia kwa nusu saa ndipo tukachukua uamuzi wa kugoma kabisa na gari itakayoingia hapa kituo haiwezi kutoka kabisa hadi kieleweke,"amesema Hamad

Kero nyingi ya muda mrefu waliaamua kuiunganisha na katika mgomo huo ni hatua ya wahusika wa kituo hicho cha kuwatoza faini ga Sh 50000 pindi wakatapobainika kunawa nyuso wakiwa msalani kwani hawaruhusiwa kufanya hivyo.

Hamad aliwataka wahusika wa kituo kuliangalia suala kwa jicho la tatu suala  la tozo ya Sh 1000  kwani huduma zinatolewa na kituo hicho haziendani na tozo hizo na badala yake waiache ya Sh 500.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post