Msanii Daz Baba
Daz Baba alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kama serikali inaweza kumruhusu kufanya kazi hiyo anaweza kutengeneza risasi pamoja na bunduki.
"Katika mchongo wa mtaani naweza kufanya biashara zozote zile kasoro biashara ya madawa ya kulevya, hivyo mimi naweza kuuza viatu, biashara za viwandani kama kutengeneza risasi na bunduki kama serikali itaniita naweza nikafanya, maana huwezi mtu kwenda jeshini kama huwezi kutengeneza silaha, saizi mimi nachokifanya ni kuwakilisha bendera yetu ya taifa"alisema Daz Baba
Msanii Daz Baba aliwahi kuingia katika tetesi za kutumia madawa ya kulevya jambo ambalo lilipelekea hata baadhi ya wasanii katika kundi lake la muziki la Daz Nundaz enzi hizo kumtenga kutokana na tetesi hizo za matumizi ya dawa za kulevya.