Wasanii wengi wa Bongo hawajielewi asema DULLY SYKES

Dully Sykes amewachana wasanii wenzake kwamba kinachowafanya washindwe katika tasnia ya muziki ni kutojitambua pamoja na kutokuwa na heshima.


Dully ameeleza hayo kutokana na uwepo wake wa kipindi kirefu bila ya kupotea au kupoteza kiwango chake katika suala zima la uimbaji tofauti na wasanii wengine ambao walikuwa pamoja kipindi cha nyuma lakini kwa hivi sasa wamepotezwa na upepo.

"Mimi najitunza, najielewa kama msanii, najitambua kwa kutengeneza 'status' yangu vizuri lakini wasanii wengi hawajitambui, mimi najitambua kuwa ni nani",alisema Dully

Kwa upande mwingine, Dully amewaasa vijana wa sasa wakubaliane na maisha wanayoishi ili waweze kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa dawa za kulevya ambapo kwa sasa imekuwa ni janga la kila mahali.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post