Watuhumiwa wengine wawili wauawa Kibiti Usiku wa kuamkia July 6, 2017


Miongoni mwa Taarifa kubwa zilizosomwa usiku wa leo July 6, 2017 kwenye habari ya Channel 10 ni pamoja na hii ya Jeshi la Polisi kuwaua watu wawili wanaodaiwa kufanya mauaji katika Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani.
Mkuu wa Operesheni Maalumu  za Jeshi la Polisi,  Naibu Kamishna wa Polis Liberatus Sabas amesema tukio hilo lilitokea usiku wa jana majira ya saa nne katika msitu wa Ngomboroni Wilayani Ikwiriri ambapo mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kushiriki katika mauaji hayo  kukamatwa na kukubali kuwaonyesha Polisi mahali ambapo hufanywa maficho ya wenzake.
>>>”Operesheni hii ni endelevu, Serikali haitakubali kuchezewa na wahuni wachache. Hawa wanaofanya matukio haya ni wachache walio wema ni wengi kwa hiyo Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Usalama tutashirikiana na wananchi ambao ni wengi kuweza kufuatilia na kuwatia mbaroni hao wanaojihusisha na matukio haya.
“Tumeshawakamata kadhaa, mahujiano yanaendelea. Vitendea kazi ambavyo ni silaha za moto nazo zimeendelea kukamatwa. Natoa wito kwa wananchi wa Wilaya za Mkuranga, Kibiti lakini pia Rufiji na meneo yanayozunguka maana taarifa inaweza kupatikana sehemu yoyote.
“Yeyote mwenye taarifa ambazo zitasaidia kupatikana wahalifu hawa ambao wanachafua taswira nzuri ya nchi yetu, Tanzania ambayo tunajua nikisiwa cha amani wanataka kutuchafua. Watupe taarifa hizo na sisi hatuta sita kuzitumia taarifa hizo na kuwatia mbaloni wahusika hawa” – Liberatus Sabas.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post