Mwalimu Nyerere Muda Mfupi Baada ya Uhuru alipata Ugeni wa Siri, Ugeni
wa Nelson Mandela. Mandela alikuwa akitaka Msaada kwa Nyerere wa
Kuanzisha Jeshi la Kupigania Haki la Umkoto We Skzwe yaani Mkuki wa
Bwana au Mkuki wa Mfalme.
Kulingana Na Kitabu cha Mandela cha Long Walk to Freedom, Nyerere
alionyesha Kusita, alimshauri asubiri asifanye jitihada za Kijeshi mpaka
Walter Sisulu aachiliwe. Wakaagana Nelson akamwambia Mwalimu atarudi
Tena na Akaenda Ethiopia ambako alikutana na Haile Selassie, Haile
Selassie alimwelewa Mandela Kwa haraka na Akampa Pesa nyingi sana tu.
Mandela akasafiri kurudi SA. Kufika huko muda Mchache akakamatwa hivyo
hakuweza Tena kuonana na Nyerere.
Baada ya Mandela Kukamatwa na Nyerere Kuona kwa Undani Uonevu wa Ukoloni
Nchi za Kusini Mwa Afrika na Ubaguzi wa Rangi SA, basi akaamua
Kujitwisha Mzigo wa Kusaidia Majeshi ya nchi zote zile na Pia sio tu
hivyo Bali kiwazi wazi akazunguka Dunia Nzima Kupiga Kelele na Pia
Kutafuta fedha za kusaidia Majeshi yale. Na mara nyingi akatumia hata
Majeshi ya Tanzania kusaidi. Hii ilimhatarisha binafsi na nchi kwa
ujumla!
Msumbiji ilipopata Uhuru Nyerere ndiye aliyewakalisha Akina Samora na
Kuwaambia wasilipize Visasi kwa Wazungu au Collaborators (Waliokuwa
wakiwasaidia wazungu) na kwa Mwongozo wa Moja kwa moja wa Nyerere
Ikaanzishwa Tume ya Ukweli na Usuluhishi (Truth and Reconciliation)
ambapo waliofanya uhalifu wa kinyama walikuwa wakikiri na Kuomba
Msamaha.
South Afrika ilipokuwa Democratic 1994 Mandela Akafuata Mfano huo nukta
kwa Nukta. Lakini Dunia Nzima ikamwenzi sana Mandela, Mandela alizikwa
na Viongozi wote Wa dunia, Ila Nyerere hakupewa heshima wala shukurani
anayoistahili na Dunia wakati wa Kifo chake.
Kila uendapo Duniani Unakuta Sanamu za Mandela, Ila Nyerere hata AU
ilibidi Mugabe aseme ikiwa Afrika haitaki Kumkumbuka Nyerere Zimbabwe
itafanya Kivyake!