Kwa baadhi ya vitendo au maamuzi yanayofanywa na huyu kiongozi kwa
kutumia cheo chake yananifanya niamini kumbe hata mimi naweza kuongoza
vizuri na kwa busara kuliko huyu.
Kitendo cha kukamata watu walioenda kufarijiana kwa msiba uliotokea eti
ni mkusanyiko usio halali eti hauna kibali, hata atumie hoja nyingi kias
gani kujisafisha ukweli utabaki palepale
Ameivua nguo serikali na mamlaka iliyomteua.
Kitendo hiki kimepanda chuki juu yake kwa sababu kuna watu wengi wapo
nyuma ya waliokamatwa mfano wale viongozi wa dini. Yaani hapo wisdom
empty hata kama itatumika jiki kusafisha hilo halitoki kwenye mioyo ya
watanzania.
Hata kama nitakamatwa mimi mtoa hoja, bado ukweli utabaki hapo na cheo
chako ni dhamana tu kesho tutakuwa wote huku mtaani. Sidhani kama
alifikiri vizuri impact ya kitendo hiki, bado najiuliza hivi
asingewakamata na kuwalaza polisi kwani kuna madhara yangetokea?
Jambo la pili ni kuhusu rambi rambi..
Najiuliza; Je, kama serikali inatumia rambirambi kinyume na matakwa ya
waliotoa rambirambi na yenyewe ipo tayari fedha inazotuma kwenye
halmashauri nchini zitumike kinyume na maelekezo?
Nakumbuka mara kadhaa waziri mkuu amekuwa akitoa onyo kali kwa viongozi
kunapokuwa na fungu fulani limetolewa kwa shughuli fulani kwamba
zitumike kama ilivyopangwa.