JE Wajua Suala Vyeti vya Bashite, Linaweza Kabisa Kumng'oa Rais Magufuli Pale Ikulu?...Tazama Hapa Uone Jinsi Inavyokuwa Kisheria.


Baada ya mahojiano ya jana ya mtu kukwepa kuzungumzia suala la kufoji vyeti vya elimu, kuna watu wanaliona hili ni jambo dogo, hivyo kujitokeza kule, kumelimaliza rasmi, no its not over until it is over!.
Japo kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT ndio mamlaka kuu kupita zote, lakini sii wengi wanaotambua kuwa mamlaka ya juu kabisa ni katiba ya JMT, na rais wa JMT, japo amejiweka juu ya katiba, lakini kiukweli yuko chini ya katiba, hivyo hili suala la mteuliwa Daudi Bashite, watu wanalichukulia kimzaha mzaha au kiutani utani, lakini tungekuwa ni nchi nyingine yenye watu wanaojielewa, jee unajua suala kama hili lingeweza kabisa kumng'oa rais Magufuli pale Ikulu kwa mujibu wa sheria akaondoka na Bashite wake?.
Tanzania ni nchi inayoongozwa na Katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Ikithibika beyond reasonable doubt kuwa Daudi Albert Bashite ni kweli alifeli kisha akafoji vyeti na kufoji jina, kujiendeleza kielimu hadi kuteuliwa, then huyu ni muhalifu kama wahalifu wengine wote, then hata rais wa JMT ampende vipi, anaweza kulazimishwa kutengua uteuzi wake kwa kuamrishwa, na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, na rais asipofanya hivyo, then rais anaweza kushitakiwa na Bunge na kuondolewa madarakani!.
Watanzania tumekuwa ni watu wa kupiga sana kelele, kulaumu, kulalamika, kushutumu bila kuchukua hatua zozote ili hali sharia zipo lakini hatuzitumii.
Sakata la Bashite ni jambo dogo sana kulishughulikia kisheria.
Hatua za kufuata.
1. Any interested party mwenye ushahidi usio shaka kuwa Daudi Albert Bashite ni muhalifu wa kufoji vyeti na kuiba jina, kupitia kwa mwanasheria binafsi anaweza kufungwa mashitaka ya kijinai dhidi ya Daudi Albert Bashite as a private investigations. Atapewa vibali vyote toka ofisi ya DPP. Kuanzisha uchunguzi.
2. Uchunguzi utaanzia kwa Daudi Bashite mwenyewe kuitwa kwa samansi ya kuhojiwa kijinai chini ya kiapo. Na akikiri tuhuma, suala la uchunguzi wa kijinai unaishia hapa, mtuhumiwa anaandika barua ya kujiuzulu na issue hii inamalizika rasmi.
3.Kwenye mahojiano hayo kama atakanusha kuwa yeye si Daudi Bashite kama alivyodanganya jana pale Star TV, then kazi ya kukusanya ushahidi inaanza kwa kutolewa samansi ya kuwahoji wahusika wote wakuu isipokuwa mke, mzazi, walimu, hospitali kufuatia kitu kinachoitwa "fiduciary relationship" ambapo sheria inampa kinga ya kuhojiwa kijinai mtu wa karibu kama mke dhidi ya mume, mzazi na mtoto, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, mwanasheria na mteja, padri na muumini etc. Hivyo kuanzia hospitali aliyozaliwa utakusanywa ushahidi wa documentary evidence aliandikishwa kwa majina gani?. Kisha Vizazi na Vifo kupata cheti cha kuzaliwa. Shule alipoandikishwa darasa la kwanza. Shule ya sekondari, Necta, vyuo, ajira alipitia, hadi idara ya uhamiaji.
4. Baada ya kukamulisha kukusanya documentary evidence, usio tia shaka kuwa Daudi Bashite amefoji vyeti. Then linafunguliwa shauri lunaloitwa "quo warranto" kuwa rais amemteua muhalifu, hivyo mahakama inajiridhisha na ushahidi uliiowasilishwa mbele yake.
5. Ndipo mahakama inatoa hati ya Quo Warranto kumlazimisha rais wa JMT, atake asitake, kutengua uteuzi wa Daudi Bashite kwa makosa ya uhalifu wa kijinai. Kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hana mamlaka ya kumteua muhalifu kwenye utumishi wa umma.
6. Kama rais atetengua uteuzi huu, then DPP atakuwa huru kumpandisha kizimbani Daudi Bashite kujibu tuhuma za jinai zinazomkabili na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.
6. Iwapo Rais wa JMT asipotekeleza amri halali ya mahakama, anakuwa amepoteza sifa za urais zilizoainishwa na katiba ya JMT ya mwaka 1977. Hivyo rais anashitakiwa bungeni na kuondolewa kwenye urais kupitia process ya impeachment.
NB.
7. Process nilizoziweka hapo ni kwa mujibu wa katiba, sasa suala kama mahakama zetu zina weza kutoa amri ya Quo Warranto au laa linabaki kwenye utelelezaji, kitu cha muhimu ni kuelimishana kuwa rais wa JMT sio kila kitu, katiba ndio kila kitu. Maadam sheria zipo, suala la sheria kufuatwa au kutofuatwa hili sio langu.
8. The same applies to impeachment process, kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa rais wa JMT, anaweza kujifanyia lolote analotaka, no! . Urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba, rais wetu atatekeleza majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, na ili kumkinga asibuguthiwe, ndio maana katiba yetu imempa kinga ya kutokushitakiwa mahakamani, lakini hakuna kinga ya kutokushitakiwa na Bunge pale anaposhindwa majukumu yake ya urais ikiwemo kututeulia wahalifu wa makosa ya jinai if proved beyond reasonable doubt, rais anashitakiwa na Bunge na anang'olewa na kuondoka na Bashite wake. Sasa suala la Bunge letu kama linauwezo wa kufanya hivi au laa, hili sio langu ni la wabunge wenyewe. Kitu cha muhimu hapa ni kujua kuwa hata rais anaweza kung'olewa madarakani na Bunge.
9. Hili sio lazima lifanywe na sheria, hata sisi media tunaweza, tukiwa na strong media yenye uzalendo usiatia shaka yenye kujua wajibu wake kwa umma, unaweza kuchunguza ukweli wa tuhuma hizi na kuziripoti, hivyo ama kumlazimisha rais wa JMT atimize wajibu wake, au kile kiti akione kichungu na kuachia kwa aibu kama ilivyowahi kutokea nchini Marekani kwa rais Richard Nikson kuachia ngazi kwenye kashfa ya Watergate.
10. Nawahakikishia hata mimi mwenyewe tuu kupitia kampuni yangu ya PPR, hili naliweza kabisa, ila kwa bahati mbaya sana, siwezi kulifanya kwa sababu kampuni yangu ya PPR, imejikita kwenye habari za kimaendeleo tuu zenye maslahi kwa taifa, yaani developmental news za Tanzania hapa tulipo, tufanyeje ili tufike kule tulikopaswa na sio habari kama hizi za vyeti vya Bashite.
Jumanne Njema.
Paskali
Chanzo - Jf

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post