SIMBA INA KIBARUA KINGINE KIZITO KIMATAIFA

 

SIMBA imetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya de Agosto ya Angola ina kibarua kingine kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda ambaye ni mzawa mechi nne kashinda zote akishuhudia kipa namba moja Aishi Manula akitunguliwa bao moja.

Ni Moses Phiri yeye amemshuhudia akifunga jumla ya mabao matano kwenye mechi hizo nne akiwa ni namba moja kwa watupiaji ndani ya kikosi cha Simba.

Droo ya upangaji wa timu ambazo zitakutana na Simba kimataifa kwenye hatua ya makundi inatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Misri.

Mechi za hatua za awali zinatarajiwa kuanza kuchezwa Februari 10 hadi Aprili Mosi 2023.

Ni timu 16 zimeshapatikana kwenye hatua hiyo ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika.

Miongoni mwa timu ambazo inaweza kukutana nazo ni pamoja na Al Ahly,(Misri), Wydad Casablanca, (Morocco), Esperance, (Tunissia) au Raja Casablanca, (morocco) ambazo zipo poti namba moja.

Poti namba mbili ni Mamelod Sundowns, (Afrika Kusini), Zamalek, (Misri), Horoya, (Guinea), na Petro Atletico Luanda, (Angola).

Poti namba 4 ni Cotton Sport, (Cameroon), Al Merreikh, (Sudan), Vipers, (Uganda) na mshindi kati ya AS Vita na RC Kadiogo, (Burkina Faso).

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post