Kumekucha...Peter Banda Asaini Miaka Mitatu Simba..Yanga Waambulia Patupu

 


Klabu ya Simba imempa mkataba wa miaka mitatu winga wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda ambaye alikuwa anakipiga  kwa mkopo ndani ya Klabu ya Sheriff ya Moldovia.

Winga huyo anahusishwa amekuja Simba kwa ajili ya kuziba nafasi ya Luis Miquissone anayetajwa kuingia anga za Al Ahly ya Misri.

Nyota huyo alikuwa ni mchezaji wa Big Bullets ya Malawi na jana alivuruga mambo kwa kile ambacho kilielezwa kuwa amepewa dili na mabosi wa Yanga.

Leo Simba wamemtambulisha rasmi kwenye ukurasa wa Instagram kwa kuandika kwamba 'Peter Banda ni Simba'.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post