AyoTV inaripoti kutokea Dodoma, Inawezekana umekutana na picha na video kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Muosha Magari wa Dodoma aliyechukua gari lililokua linatakiwa kuoshwa na kuliendesha lakini kwa bahati mbaya alipata nalo ajali baada ya kuingia Barabarani.
Sasa Ayo TV ilifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi wenzake japo wameomba wasionekane kwenye camera wala kurekodiwa, wamesema ni kweli wanamtambua Muosha Magari huyo na hajachanganyikiwa baada ya kuliangusha Gari aina ya Ford Range kama inavyosemekana bali ni mtu ambaye wanadai ana tatizo la akili kutokana na baadhi ya matukio ambayo amekuwa akiyafanya siku za hivi karibuni.
AyoTV inaendelea kumtafuta Mwenye Car Wash na Mmiliki wa gari hili ili kufahamu zaidi.