Waziri Aendesha Kikao na Mtoto Mgongoni

waziri wa elimu wa Sierra Leone, David Moinina Sengeh, amegeuka gumzo mtandaoni baada ya kuendesha kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao akiwa amembeba mtoto na mbeleko mgongoni.

Sengeh mwenye umri wa miaka 33 ameiambia BBC kuwa aliamua kumbeba mwanae mwenye umri wa miezi 10 wakati akiongoza kikao ili kutoa mfano kwa wanaume wengine nchini humo.

“Wanawake wengi hufanya hili kila siku, lakini ni jambo la kawaida sana kiasi kwamba hatulizungumzii kabisa. Kama angelikua ni mke wangu aliyefanya hivyo Twitter hii isingezungumziwa kabisa ,” Amesema waziri huyo.

Ameeleza kuwa alikua jikoni nyumbani akimlisha mwanae Peynina alipoanza kushiriki katika kikao cha video kupitia programu ya intaneti ya Zoom na alibaini kuwa alikua anaonekana mwenye usingizi, kwa hiyo akaamua kumbeba mgongoni ili kuendelea na mkutano wa kazi.

Amesisitiza kuwa “Picha hii iliwalazimisha kujifikiria, inawaonyesha kwamba inawezekana kuwalea watoto wao , “Nina marafiki ambao hawajawahi hata mara moja kuwabadilishia nepi watoto wao, na hata hawaelewi ni vipi hilo linawezekana,”

Ikumbukwe kuwa Sierra Leone ina visa 124 vya corona vilivyothibitishwa na imekwisharekodi vifo saba kutokana na janga hilo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post